<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><title>Bwana Wa Mabwana TZR62</title>
<lyrics>[V1]
 Bwana wa mabwana,
 Mwenye nguvu sana
 Twakusihi:
 Neno la milele
 Na liende mbele,
 Waongoke tele
 Kwa Mwokozi.

[V2]
 Tunaowaona
 Wanavyopatana,
 Kulipinga,
 Hawataliweza
 Neno, kulitweza:
 Huwaje! Kucheza:
 Na upanga?

[V3]
 Heri wajitunze
 Ili wapatane,
 Na Mwokozi;
 Watafute sana,
 Wapate kuona,
 Yesu kuwa Bwana,
 Mkombozi.

[V4]
 Mungu awaita
 Wasije kukuta
 Pigo lake;
 Hakuona vyema
 Wakose uzima,
 Awape rehema,
 Waokoke.

[V5]
 Mwenye utukufu
 Tunamshukuru
 Yeye pweke!
 Nasifiwe sana,
 Baba, naye Mwana,
 Na wa tatu tena
 Roho yake.</lyrics>
<hymn_number>62</hymn_number>
</song>